Polisi Wanasa Zaidi Ya Lita 300 Za Pombe Haramu Taita Taveta

Naibu kamishena wa Mwatate Kenneth Muriungi katika kituo cha polisi cha Mwatate./Solomon Muingi
Naibu kamishena wa Mwatate Kenneth Muriungi katika kituo cha polisi cha Mwatate./Solomon Muingi
Polisi huko Mwatate kaunti ya Taita Taveta wamenasa zaidi ya lita 350 za pombe haramu aina ya M'bangara ikiwa zimefichwa katika machimbo ya migodi huko Mkuki.

Naibu kamishena wa Mwatate Kenneth Muriungi anasema watu 24 walitiwa mbaroni katika operesheni hiyo inayolenga kukabiliana na uuzaji na unywaji pombe haramu katika eneo hilo.

Muriungi anasema operesheni hiyo inayoongozwa na maafisa wa usalama na nyumba kumi imenasa zaidi ya lita 15,000 katika eneo la Mwatate pekee tangu mwezi jana.

Ameitaka jamii kushirikiana na maafisa wa usalamu kukabili kero la utumizi wa dawa za kulevya huku akitoa onyo kali kwa watu wanaojihusisha na biashara hiyo kuwa watachukuliwa hatua kali za kisheria.

-Solomon Muingi.