Polisi wapata mifuko ilibeba shilingi milioni 72 za wizi

G4S
G4S
Polisi wamepata masanduku na mifuko 13 ya kubebea pesa iliotumika katika wizi wa pesa siku ya Alhamisi na watu waliojifanya maafisa wa kusafirisha fedha.

Wezi hao walifanikiwa kuiba jumla shilingi milioni 72 zilizokuwa zatarajiwa kusafirishwa kutoka makao makuu ya kampuni ya ulinzi G4S katika barabara Witu kupelekwa kwa mashine ya ATM ya Benki ya Standard Chartered katika eneo la Nairobi West.

Masanduku na mifuko hiyo ilipatikana usiku wa kuamkia Ijumaa katika msitu wa Thogoto, kaunti ya Kiambu. Polisi walipata masanduku na mifuko ya benki za Stanbic, KCB na Barclays.

“Iliripotiwa na mkaazi mwendo wa saa sita usiku siku ya Ijumaa kwamba palikuwepo masanduku yaliokuwa yamevunjwa na mifuko ya fedha kutoka benki mbali mbali,” kulinagana na maelezo katika sajili ya polisi namabari ripoti 33/5/2019.

Watu waliojifanya maafisa wa kusafirisha pesa walitoweka na kiasi kikubwa cha pesa hizo na kutokomea baada ya kuziweka kwa gari aina ya Toyota Noah. Bidhaa zingine zilizopatikana msituni ni simu za mkononi, kadi ya simu yenye nambari 89254021104175661927 na jaketi jeusi la G4S.