Polisi watawanya watu eneo la Mlango Kubwa kwa kujaribu kuingia Eastleigh

EYm5MNEWkAI64dR
EYm5MNEWkAI64dR
Maafisa wa usalama asubuhi hii wamelazimika kutumia vitoa machozi ili kuwatawanya wakaazi wa mtaa wa Mlango Kubwa waliokuwa wanataka kuvuka vizuizi vilivyowekwa na polisi kuvuka katika mtaa wa Eastleigh uliofungwa na serikali kama njia ya kupunguza usambaaji wa virusi hatari vya corona.

Ni mara ya pili sasa polisi kulazimika kuwatanya wakaazi katika maeneo hayo ambao wamekuwa wakijaribu kwende kiunyume na sheria kuhusiana na utaratibu uliowekwa na serikali.

Mtaa wa Easytleigh na Mji wa Kale Mombasa uliendelea kufungwa na serikali hadi Juni tarehe 6.

Kwengineko ni kuwa, mwili wa mwanafunzi wa darasa la tano katika mitaa ya Kibra jijini Nairobi umetolewa katika Kidimbwi kilichojaa maji eneo la Soweto.

Shughuli ya kuopoa mwili huo imefanikishwa na wakaazi wa mtaa huo.