Polisi anayedaiwa kuhusika kwa mauwaji ya George Floyd aomba msaada wa kulipia dhamana

jsvZJT5H.jfif
jsvZJT5H.jfif
Mmoja wa maafisa wa polisi aliyehusika katika mauaji ya Mmarekani mweusi mjini Minneapolis George Floyd anaomba msaada ya kifedha ili aweza kulipa dhamana ya kuachiliwa huru.

Thomas Lane anaamini kuwa raia na wahisani watajitokeza na kumchangia KSh 106 milioni zinazohitajika ili kulipa dhamana yake.

Kupitia kwa tuvuti iliyowekwa na familia yake, Lane alijaribu kila awezalo kuyaokoa maisha ya Floyd ila mwenzake Derek Chauvin hakutaka kumsikiza.

Familia ya Lane ilihoji kuwa, alikuwa afisa wa kwanza kuitisha ambulensi baada ya Floyd kupoteza fahamu na hata alijaribu kumfanyia huduma ya kwanza.

Kwa mujibu wa taarifa ya familia yake, Lane mwenye umri wa miaka 37 alikuwa amehudumu katika mitaa kwa siku nne pekee na alikuwa anafuata masharti yaliowekwa tayari.

Mshukiwa mkuu katika mauaji ya Floyd Derek Chauvin amepatiwa dhamana ya dola milioni moja na huenda akaachiliwa huru.

Aidha, mshukiwa huyo amepatiwa masharti makali ikiwemo kutoruhusiwa kuzungumza na familia ya marehumu Floyd wala kufanya kazi katika idara yoyote ya afya.