Pombe inawapotezea muda na pesa zenu; Frasha awambia walevi

Kiongozi wa chama cha Maendeleo Chap Chap, Frasha amesema kuwa ameachana na pombe kabisa na sasa anataka vijana waachane na ulevi kabisa kama yeye.

Frasha ambaye hivi karibuni amekuwa akiwarai vijana waache pombe hivi karibuni amekuwa mlevi kwa zaidi ya miaka kumi na mitano sasa.

"Nilijipa changamoto ya kususia pombe kwa siku 40 sasa kila mwaka na sasa nimegundua umuhimu wa kuachana na ulevi," Frasha alieleza Word Is siku ya Jumanne. Frasha anasema kuwa upo wakati alitumia hela zaidi ya elfu mia tano chini ya mwezi mmoja.

"Jinsi mtu anavyozidi kukua ndivyo ajuavyo kuwa vitu vingine havina umuhimu wowote maishani mwako kwani vinaharibu wakati wako, pesa yako pamoja na kukupotea fahamu bure."

Frasha alisema kuwa anajutia kuhusu pesa alizotumia kwenye ununuzi wa pombe," Hakuna jambo nzuri kuhusiana na pombe. Kazi kubwa ni kukuharibia wakati, inakuumiza mwili wako bure pamoja na kukupotezea mambo ya maana."

Frasha amewapa changamoto kwa kuwaambia wafikirie mahali watakuwa miaka miwili ijayo na wajue mahali watataka kua miaka miwili ijayo kuanzia sasa,"Nimegundua kuwa pombe ipo kila siku na itaishi kuwako licha ya jambo lipi liyokee.Mke wangu haniamini na hivyo ameniambia nimpe mude kwai bado anafikiria mimi ni mlevi."

Frasha kwa sasa anaendelesha chama chake cha Frasha HIV Foundation ambacho kinawasaidia na kuwashauria watu wanaougua ugonjwa wa ukimwi.