Pozze amuomba Alaine amrudie

Willy Paul almaarufu aliyejulikana kama Pozze amemuomba mwanamziki wa kijamaica Alaine amrudie.

Pozze amesema kuwa Alaine alimzui kwenye mitandao yote ya kijamii yake pamoja na kumlisha 'blueticks' anapomtumia ujumbe mfupi, hivyo basi kufanya mambo kuwa magumu kwake kujua yanayoendelea.

Willy Paul pamoja na Alaine walitetemesha dunia kwa kibao chao cha 'I Do' mwaka uliopita. Wimbo huo ulimletea Willy Paul sifa nyingi hadi kufikia wakati wakenya wakasema kuwa huenda wawili hao wanachumbiana.

"Tulikuwa na uhusiano mzuri sana.Kupatana nawe ilikuwa kama ndoto iliyotimia maishani mwangu...ukimwona mwanaume akisema jambo kama hili basi jua anamaanisha kitu kizuri. Niliamka leo nikihisi jinsi ulivyokuwa unazipenda picha zangu.Mie sithani kama nimekukosea kwa njia yoyote ile.

Sababu kuu ya Willy Paul kuzuiwa na Alaine ni Nandy ambaye hivi majuzi waligonga vyombo vya habari baada ya kupiga shoo moja huku wakiwa fanya colabo moja ya nguvu.

Hata hivyo, kulingana naye Willy, Nandy ni rafiki tu ila hamna jambo kubwa baina yake na mkali huyo.

Willy Paul almaarufu kama Pozze amemuomba mwanamziki wa kijamaica Alaine amrudie. Pozze amesema kuwa Alaine alimzui kwenye mitandao yote ya kijamii yake  pamoja na kumlisha 'blueticks'.

Alaine alikuwa humu nchini hivi majuzi kupanga shoo ya Morgan Heritage na hakumtafta Willy Paul jambo lililomkosesha Pozze usingizi.