Premonition? Zeddy alizungumzia kifo cha Kasee miezi,8, iliyopita

Mcheshi Zainabu Zeddy almaarufu Zeddy alionya kwamba kutakuwa na kifo cha mcheshi na kuwa tasnia ya ucheshi haitawacha kuomboleza kama tasnia hiyo haitaingililia kati na kutatua shida zinazowakumba wacheshi kama vile kuwa na mawazo mengi.

Miezi minane iliyopita, familia ya ucheshi ikiomboleza kifo chake mswahili Njenga, Zeddy alisema kuwa kusongwa kwa mawazo kwa wacheshi ndiko kumechangia katika vifo vya wacheshi wengi kwa sababu ya hali duni ya kifedha.

"Sijui nianzie wapi aki! Nko na makasiriko mengi saa hii 😥 tutapoteza Wasanii wangapi juu ya Depression!!! Rip Bro😪 ingawa sijui kilicho kufika but najua depression imechangia sana. Ombi langu kwa Jamaa na Familia tuoneni kama nyinyi tu msiweka matumaini mengi kwetu sababu tunatafuta Riziki kama nyinyi tu!" Alizungumza Zeddy.

Mcheshi Mswahili Njenga almaarufu Anthony Njenga alipatikana akiwa ameaga dunia mwaka jana Novemmba tarehe,7, baada ya kudaiwa kuwa aligongwa na gari moshi.

Pia Zeddy alisema kuwa kuna mcheshi ambaye amerudi na nyuma kwa anataka kumuona kabla ya kitu kibaya kutokea.

“KWA SASA NAMTAFUTA MMOJA WETU KASEE UKIWA NA HABARI KUMHUSU DM PLIZ..BEFORE RIP NYINGINE NI HAYO TU. RIP NJENGA MSWAHILI KOMA THAYO JABA🙏."

Taerehe 28 Juni, Kasee alipatikana kwenye barabara akiwa ameaga alipokuwa anaelekea nyumbani kwake Kinoo, mwili wake ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Chiromo.

Polisi bado hawajabaini kiini cha kifo chake bali wanazidi kufanya uchunguzi.