Prezzo amkejeli Jaguar kwa matamshi ya chuki

prezzo na jaguar
prezzo na jaguar
Baada ya mwanamuziki maarufu na mbunge wa starehe "Jaguar " kukamatwa na polisi, Rafiki wake wa karibu na Mwanamziki, Prezzo amejotekeza hadharani na kumkejeli Jaguar kwa maneno yake makali aliyotoa siku ya jumatatu maeneo ya Gikomba kuhusu wafanyabiashara kutoka mataifa jirani Tanzania na Uganda.

"Ukitembelea masoko yetu hapa mjini nairobi kuanzia Gikomba utapata kwamba yamechukuliwa na Watanzania na Waganda. Sisi hatuongei kuhusu wachina sita."

Katika mtandao wake Prezzo alimjibu jaguar kwa kusema," Kakangu sijui nianzie wapi lakini matamshi yako ya jana hayakuleta shangwe kamwe.

Maana ya kiongozi ni kuwaongoza watu kwa njia mwafaka na sio vita hasa sasa kwa majirani zetu Tanzania na Uganda. Sisi wote tunatafuta riziki duniani ili tueze kulisha familia zetu nakui jenga nchi yetu.

Kuna wakenya wanatafta riziki nchi zingine mbali na Kenya so uamuzi wako wa kuipa serikali masaa ishirini na manne kuwatoa wafanyakazi wenye biashara zao ambao sio wakeny ulichemsha."

Hata hivyo Prezzo alimtakia kila la heri Jaguar huku akuimweleza kua atamwombea ili aweze kuwa kiongozi wa kutegemewa na wananchi wote .