Producer Magix ampa Harmonize masaa 48 aombe msamaha, atishia kutoa audio

Producer Magix Enga amezidisha juhudi zake za kuona kazi za wasanii hapa nchini zimeheshimika.

Magix baada ya kuifuta ngoma ya Harmonize YouTube sasa amemjia juu na kuamua kuifuata mpaka audio.

Enga amesema kuwa kuna dharau kubwa ya wasanii kutoka bongo Tanzania kutoheshimu kazi zinazotoka Kenya.

Mkwaju huu ulikuwa ushaanza kupata upigwaji mkubwa redioni hapa nchini na kushika nafasi za kwanza katika mtandao wa YouTube.

Ikumbukwe kuwa Harmonize amefanya ziara kubwa Afrika mashariki akipigia uno kampeni kubwa.

Harmonize alipewa makataa ya siku 7 kuomba msamaha ili ngoma isifutwe.

Magix sasa amesema kuwa anampa masaa 48 kuomba msamaha ama aitoe na audio ya UNO.

Kulingana na Magix, mdundo ulioibiwa ulikuwa wa ngoma ya King Kaka na Kristoff.

Producer huyu alirekodi kipande cha video akilalama kuhusu wizi wa mdundo huo.