Producer mkubwa nchini Magix Enga azima UNO ya Harmonize,atoa onyo kali

Screenshot_from_2019_11_21_11_03_13__1574323509_22539
Screenshot_from_2019_11_21_11_03_13__1574323509_22539
Mtayarishaji mkubwa wa ngoma nchini Magix Enga ametoa onyo kali kwa msanii yeyote anayeiba midundo yake.

Magix Enga ametoa onyo hii katika mtandao wake maridhawa wa Insta.

"1 Week Imeisha and The song Uno is no longer on YouTube Don’t sample magix Enga Beats. I repeat, dont! Like I said i’m not going to allow this to happen not in 254 🇰🇪..." Alifoka Enga.

Ngoma ya UNO ilikuwa inafanya vizuri katika mtandao wa Insta kabla ifungiwe.

https://www.instagram.com/p/B5FVhVtHSS9/

Mkwaju huu ulikuwa ushaanza kupata upigwaji mkubwa redioni hapa nchini na kushika nafasi za kwanza katika mtandao wa YouTube.

Ikumbukwe kuwa Harmonize amefanya ziara kubwa Afrika mashariki akipigia uno kampeni kubwa.

Meneja wake pia ametoa tamko kuhusu kufungiwa kwa ngoma hii.

"Tumepata taarifa kutoka YouTube Kwamba ,mtu mmoja ambae inasemekana kutoka nchi jirani Kenya,ametuma barua pepe kudai umililiki wa wimbo wetu Pendwa..."

Inashangaza zaidi kuona meneja wa Konde Gang hamfahamu Magix Enga.

Meneja huyu aidha amesema wako tayari kufuata taratibu za YouTube.

"Aidha kwa taratibu zao YouTube ni lazima wauweka private wakati wakiendelea na taratibu za kujiridhisha juu ya madai hayo..."

Kulingana na Magix, midundo ya UNO imeibiwa kutoka kwa ngoma ya Dundaing.

Ngoma ya Dundaing ilifanyika hapa nyuma huku King Kaka, Kristoff na Magix Enga.

Enga alikerwa kwa kuona hatimiliki zake za midundo hii zikitumiwa bila idhini na kutoa makataa ya wiki moja kwa Konde Gang kuomba msamaha.