“ Baada ya mtoto kuzaliwa ,marehemu alikubali kwamba mtoto alikuwa wake na kuchukua majukumu ya uzazi kwa kushughulikia maslahi yake na yangu alipokuwa hai’ Thumbi amesema .‘Okoth alikuwa baba mzuri na kabla ya kifo chake alikuwa akitekeleza majukumu yake kama baba ipasavyo kwa kuhakikisha kuwa mwanawe ana nguo ,burudani na karo ya shule miongoni mwa gharama nyingine’ ameongeza Thumbi . Mwakilishi huyo wa kaunti ameserma alikuwa akiwasiliana na Okoth mara kwa mara alipokuwa akiugua na nyakati za mwisho za maisha yake . ‘Alitaka kwamba Mrithi wake wa pekee aliyebeba jina lake atunzwe na kutambuliwa ili kuendeleza kizazi chake , jambo ambalo aliniambia na pia kuwafahamisha ‘watu wa karibu wa familia yake’ Thumbi amesema .Thumbi ameongeza kwamba mtoto huyo anafahamika sana na watu wa familia ya Okoth akiwemo nyanyake ambaye amekutana na kutangamana naye kwa muda tangu mjukuu wake alipozaliwa .
Kupitia wakili Elkana Mogaka, amesema mtoto huyo amenyimwa haki ya kuhusishwa katika maazishi ya babake na tamaduni zote zinazoambatana na shughuli hiyo . “ Mamake Okoth na mkewe kwa bahati mbaya wamemtenga Muthoni(Thumbi) katika mipango ya maazishi na wamefahamu tu kuhusu shughuli hizo kupitia magezetini na vymbo vya habari’ Mogaka amesema . Pia amesema familia hiyo iliamua kuuchoma mwili wa Okoth ili kuharibu DNA miongoni mwa sababu nyinyine kwa lengo la kuondoa kabisa uwezekano wa kupatikana ushahidi kwamba Okoth ndiye baba ya mtoto huyo .
Mtoto huyo anatarajiwa kuripoti shuleni Septemba mosi ,ilhali hakuna mawasiliano yaliyotolewa kuhusu karo yake ya shule .Mama mtoto anataka mahakama kuiagiza familia ya Okoth kupitia mali ya mbunge huyo kulipa kiasi kikubwa cha fedha kwa wakati mmoja zitakazotumiwa kama karo ya shule ya mtoto huyo . Thumbi amemshtumu mkewe Okoth Monica kwa kumbagua mtoto wake akisema kwamba ameonyesha ishara za ubaguzi wa rangi dhidi ya mtoto pekee ambaye ni mrithi halali wa marehemu .Mkewe Okoth Monica ni mzungu .