Quarantine? Meneja wa Tanasha akana madai kuwa staa huyo yupo karantini

Screen-Shot-2020-03-20-at-5.17.29-PM
Screen-Shot-2020-03-20-at-5.17.29-PM
Meneja wa Tanasha Donna Castro amekana madai kuwa staa huyo yuko katika karantini wala katika kitengo cha kipekee kwa ajili ya virusi vya corona.

Hii ni baada ya nduru za ripoti kusema kuwa Tanasha alivunja na kukaidi amri ya kutotoka nje na kwenda kujivinjari na kusherehekea siku ya kuzaliwa ya mwanabiasha Tim Matiba.

Meneja wake akizungumza alisema,

"WHERE DID YOU GUYS EVEN GET THAT INFORMATION FROM?" Castro Aliuliza.

Meneja huyo alikana madai hayo na kusema kuwa hamna kitu kama hicho na alikuwa na Tanasha jana nyumbani kwake.

“THERE IS NOTHING LIKE THAT. AS A MATTER OF FACT, I WAS WITH HER IN HER HOUSE YESTERDAY.” Alisema.

Kupitia mtandao wa kijamii wa instagram, Tansha aliposti video akiwa katika sherehe hiyo, pia alipost akiwa na msanii Nandy video ambayo imeenea sana katika mtandao huo.

Kulingana na Tanasha, wanawake wengi wanapaswa kung'aa na kufuata ndoto zao katika sanaa ya muziki.