R.I.P: Familia kuomboleza kifo cha rubani wa ndege ya Ethiopian Yared

Yared Mulegeta
Yared Mulegeta
Anga ndio iliweza kuwa kikomo hasa kwa rubani wa ndege ya Ethiopian ya aina ya ET302 ambayo ilifanya ajali jumapili mwendo wa asubuhi.

Ni ajali ambayo iliweza kuwauwa abiria 157 wote huku rubani Yared Mulegeta akiwa miongoni mwao.

Familia ya Yared wanateketea na makali ya uchungu mioyoni mwao, kwa kifo cha ghafla cha rubani huyo na kumsimulia kama mwenye alikuwa na kipaji cha pekee.

Aliweza kupandishwa cheo hadi kuwa rubani mkuu wa ndege za Ethiopian akiwa na miaka 29, aliweza kuwa mkweli na kuipenda kazi yake, kisha aliweza kukumbana na kifo akiwa anafanya kazi yake.

"Kipaji na nia nzuri na kubwa ya Yared ilionekana wakati alipopandishwa cheo hadi rubani mkuu, akiwa na bado miaka 29." Alisema mpwa wa Yared anayefahamika kama Zainab Dahab.

Kauli ambayo familia ya Yared walisema na gazetti la star walisema kuwa, ndiye alikuwa rubani mwenye miaka chache huku ikiwa ni historia katika kampuni ya ndege ya Boeing 737.

Yared alizaliwa na wazazi wa nchi tofauti baba Getachew Tessema akiwa ni wa Ethiopia, huku mama yake Rayan Shapi akiwa ametoka nchi ya Kenya.

Wazazi wake wakiwa ni madaktari wa meno ambao walikuwa wamestaafu.

Yared alienda katika shule ya msingi ya Allen Grove mjini Nairobi na kisha kuenda tena katika shule ya msingi ya Oshwal, aliweza kurudi Ethiopia na kuenda shule ya upili ya Prestigious Ethiopian Aviation Academy.

"Yared alitaka kuwa rubani tangu utotoni, alikuwa mwenye bidii, alikuwa anatimiza na kukamilisha ambacho macho yake yalikuwa yameona, tumepoteza ntota angavu, alikuwa anang'aa siku baada ya ingine." Daham alisema.

Aliweza kuitimu katika shule hiyo aliokuwa ameenda kusomea kazi ya ndoto yake mwaka wa 2010, na kukuwa na bahati kubwa kwa kupata kazi katika kampuni ya ndege ya Ethiopian mwaka huo.

Alifanya kazi tangu mwaka huo hadi wakati wake wa mwisho alipofanya ajali Jumapili.

"Baadhi ya maripota wanasema kuwa Yared alikuwa mwananchi wa Ethiopia, si ukweli Kenya ni nyumbani kwake na familia yake,

"Yared  alipenda Kenya na alikuwa nchini Ethiopia kwa ajili ya kazi pekee." Aliongea mpwa wake.inaishi katika kaunti ya Mombasa eneo la

Familia yake wanaishi Springs Valley na familia kubwa kuishi mjini Mombasa, eneo ambalo maombi ya mwendazake Yared yanafanyika.