Radio Africa kuzindua wimbo mpya wa Sauti Sol

Bendi ya muziki wa Afro-pop Sauti Sol inajiandaa kuzindua kibao kipya mnamo Mei 22. Kibao hicho kinafahamika kama 'insecure'. Sauti Sol wameshirikiana na Radio Africa group kutoa kibao hicho ili kujitayarisha kwa albamu yao mpya itakayozinduliwa Juni 5, 'midnight train'.

Mashabiki wa Sauti Sol wanatarajiwa kuuskiza uzinduzi huo kupitia Radio Jambo, Classic 105, Kiss 100, Smooth fm na Homeboyz Ijumaa asubuhi.

Kibao chao cha 'Suzanna' kimetamba sana katika mitandao ya kijamii huku kikifikisha mashabiki millioni tisa katika youtube.

Kibao cha 'Brighter days' kilichotolewa Aprili 17  tayari kina mashabiki zaidi ya millioni 1.2.

Bendi ya Sauti Sol ilisema kuwa wakati huu ambao nchi inapitia janga la corona wasanii wameathirika pakubwa na hata uchumi wa nchi kuzorota huku mamilioni ya watu wakipoteza ajira.

"It has forced us to not only postpone and/or cancel all local and international performances but also to isolate at a time we need to be together preparing for the launch and eventual performance and touring of our new album

It is the expectation of our fans and stakeholders that we launch this album with a concert/performance regardless of the circumstances."  wanachama wa bendi hiyo walisema.

Baadhi ya watangazi wa Radio Jambo walizungumzia hofu zao maishani.

"Ninahofia kesho watoto wangu watakuwa akina nani na pia kesho nikiamka afya yangu ni duni." Massawe Alisema.

Ghost naye alikuwa na haya ya kusema,

"Mimi kama baba nahofia nikirudi nyumbani watoto wanakuuliza baba vipi, labda karo ya shule hujamaliza kulipa, huwezi wanunulia chakula mambo kama hayo yananipatia mimi kiwewe."Alizungumza Ghost.

MHARIRI; DAVIS OJIAMBO