'Rafiki yangu' Jacque Maribe anendelea kupigana - Dennis Itumbi anong'ona

Mtangazaji wa runinga ya Citizen Jacque Maribe aliweza kukumba na kesi akiwa na mpenzi wake Jowi ya kumuuwa Monica mwaka jana.

Rafiki yake Dennis Itumbi aliweza kuenda jana katika mahakama wakati wa kusikizwa kwa kesi ya mshukiwa Jacque Maribe huku akienda katika mtandao wake wa kijamii wa Instagram kuwa rafiki yake anaendelea kupigana.

Aliweza kuandika na kusema;

"My friend Jacque Maribe fights on in court. Eventually Facts. Evidence and the Law will carry the day," Aliandika Dennis.

Hakuweza kutia kikomo katika ujumbe wake bali aliongeza na kusema kuwa

"But let justice roll down like waters and righteousness like an ever-flowing stream," Dennis aliongeza.

Mmoja wa mashabiki aliweza ona picha zao wakiwa pamoja katika mtandao huo na kuwaambia kuwa wanakaa vizuri sana pamoja na wawache haki itendeke.

Katika kesi hiyo Jacque aliweza kuomba mahakama aweze kurudishiwa gari lake ambayo iliweza kushikwa wakati wa kisa hicho, huku ikidaiwa kuwa ndio iliweza kutekeleza mauaji hayo.

Mahakama iliweza kukataa ombi la Jacque Maribe na kusema kuwa gari hilo ndilo lina ushahidi wa mauaji hayo.

Katika kiapo kilicho letwa mbele ya mahakama jana, kilisema kuwa mchunguzi Maxwell Otieno alisema kuwa gari hilo na rununu ya simu zitaweza tumuwa kama ushahidi wakati wakesi ya mashtaka hayo.

Kwa maana bidhaa hizo zitatumika katika maonyesho, mahakama hawakumkamata na mamalaka ili ziweze kuachiliwa.

Jaji aliweza kuelekeza makundi hayo mawili yaweze kuja mahakamani machi 13, ili kuja kupambana na kiambo walichokuwa wameandika.

Katika Ujumbe huo wa Dennis Itumbi katika mtandao wake wa kijamii mashabiki waliweza kuchangia kwa maoni tofauti.

Yafuatayo ni baadhi ya maoni ya mashabiki;

esirmorgan: Everything happens for a reason......its gonna be over soon....👊

deekaris: Monica was murdered nobody remembers her name now. When you post pictures of Jacque and you on friendship. If Jacque is found guilt by the same justice I hope you will accept that too. Monica is a person too who deserves justice too.

shee2554: Justice to maribe...kumbuka jowie pia