Rai Uhuru Kenyatta awataka Machifu kuwajibikia ongezeko la Mimba za mapema

Rais Uhuru Kenyatta sasa ameunga mkono hatua ya mratibu wa serikali George Natembaye katika eneo la Rift Valley kuwa machifu ndio watakaowajibikia kujibu madai ya ongezeko la mimba za Mapema miongoni mwa wasichana wa umri mdogo.

Kenya amesema ni sharti machifu kote nchini kuwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa wanabaini wale wanaowapachika mimba wasichana wa miaka midogo.

“You as the area chief will have to answer, where were you when all this was happening?” “People must be disciplined, how do we allow people to go around impregnating young girls, and we do not say anything? We are going to wait for the DNA and those people will pay,” Kenyatta

Wito huu unajiri huku visa vya wasichana wa umri mchanga kupachikwa mimba vikiongezeka nchini baada ya shule kufungwa kutokana na hofu ya corona.

Mwezi jana ,Natembaye aliwataarufu machifu kutoka ukanda wa Rift Valley kuwa ,wao ndio wataeleza kuhusiana na wasichana ambao watapatikana wakiwa wajawazito eneo hilo.