taka.taka

Raia wa Uganda washutumiwa kutupa taka taka upande wa Kenya

Usimamizi wa mji wa Busia umelalamikia hatua ya Raia wa nchi jirani ya Uganda kutupa taka taka upande wa Kenya na kupelekea serikali ya kaunti ya ka Busia kugharamia kuzoa taka hizo pasi na kuwatoza ushuru.

Msimamizi wa mji huo Ken Nabulindo amesema raia wa Uganda wanatumia kuwepo kwa sehemu wazi kwenye mpaka wa Kenya na Uganda upande wa Kenya yaani security zone kutupa taka taka ili hali hawatozwi ushuru huku akiitaka serikali ya kitaifa kuruhusu serikali ya kaunti kuboresha sehemu ya kufanya kuwa soko wazi.

-Leonard Acharry

Photo Credits: RNZ

Read More:

Comments

comments