Raila amfurusha Pareno katika mageuzi ya kuboresha ODM

Parenno
Parenno
Katika kinachoonekana kama matayarisho ya uchaguzi mkuu wa 2022 chama cha ODM kimeunda bodi mpya ya uchaguzi na  kamati ya nidhamu huku bodi ya zamani ikifurushwa baada ya lalama nyingi kuzuka wakati wa uchaguzi wa mwaka wa 2017.

Kiongozi wa chama hicho Raila  Odinga siku ya Jumanne  aliifurusha bodi ya zamani ya uchaguzi iliyokuwa ikiongozwa na Judy Pareno  na ambayo ilishtumiwa kwa kusimamia vibaya mchakato wa uchaguzi wa kuwateua wagombeaji wa ODM   na kuvuruga  matokeo ya chama katika uchaguzi mkuu  uliopita

Catherine Mumma aliywahi kuhudumu katika tume iliyovunjiliwa mbali ya utekelezaji wa katiba sasa ndiye mwenyekiti mpya wa bodi ya kitaifa ya uchaguzi . wengine katika bodi hiyo ni   mbunge wa zamani wa wajir kusini Abdulahi Diriye, Richard Tairo, Syntei Nchoe  na  Emily Awita.

Prof Ben Sihanya anachukua usukani kama mwenyekiti wa kamati ya nidhamu kutoka kwa  wakili  Fred Athuok. Kamati hiyo ya nidhamu pia ina sura mpya kama vile  Ramadhani  Abubakar, Mumbi Ngaru, Seth Kakusye  na  Dr Florence Omosa.

Hatua ya Raila kumteua Mumma katika bodi ya uchgauzi inalenga kutumia ujuzi wake katika sheria kutekeleza ripoti ya tathmini yenye mapendekezo mengi ya kuboresha matokeo ya uchaguzi  ya chama hicho  .

Mumma  aliongoza kamati iliyotoa mapendekezo na kuikosoa vikali bodi ya zamani kwa kutumia ghasia ili kuwapa vueti wagombeaji ambao hawakuwa na umaarufu mashinani .

Bodi hiyo mpya itatoa ratiba na kuandaa uchaguzi wa chama hicho ambao uliahirishwa kwa sababu ya janga la Covid 19