Oscar Sudi adai kuwa Raila huabudu Shetani

Oscar Sudi
Oscar Sudi
Mbunge wa Kapseret  Oscar Sudi  amedai kuwa kinara wa ODM Raila Odinga 'anaabudu shetani ' baada ya Jubilee kubwagwa katika uchaguzi mdogo wa Kibra.

"Kabla ya uchaguzi wa Kibra, Raila alikuwa amesafiri Nigeria, na kichwa chake kimezingirwa na uchawi," Sudi alisema haya katika halfa ya kuchangisha pesa katika Kanisa la Kikatoliki la St. Patrick.

Alisema kwamba Raila alitumia nguvu za giza hili kuhakikisha jamii za  Kalenjin, Kikuyu, Kamba na Luhya kupigia kura wagombeaji wao.

"Mzee huyu anaabudu shetani na atashindwa kwa jina Yesu...wangapi wananiunga mkono, inueni mikono juu pamoja nami?" Sudi alisema.

Mbunge huyu alisema Raila ni "mkoloni mwafrika' huku akimlaumu kwa maendeleo duni katika eneo zima la Kibra.

"Alihudumu kama Mbunge wa Langata kwa miaka 20 na akawa waziri mkuu kwa miaka mitano na hadi wa sasa watu wa Kibra wanakosa vyoo huku wakitumia mifuko ya plastiki," alisema.

"Kama viongozi wachanga katika nchi hii, lazima tupigane kwa hali na mali hadi huyu mzee anayeabudu shetani astaafu,'' alisema.

"Tunataka Kenya kuhakikisha kwamba kila kabila la Kenya laweza kuishi na kufanya kazi katika kila eneo la nchi hii bila uoga wowote au kutishiwa,'' alisema.

Sudi alimshauri kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka na mwenzake wa Ford Kenya Moses Wetangulia kutema muungano wao na Raila na kuungana na naibu rais William Ruto ili kuunda serikali 2022.

''Raila haendi kanisa, hatoi pesa za mchango makanisani na misikitini....atapata vipi baraka za Mungu ?" Sudi aliuliza.