Raila awataka wana Kibra kulinda "Bedroom" yao

kibra
kibra
Kiongozi wa ODM Raila Odinga amewataka wapiga kura wa Kibra kulinda kura zao katika uchaguzi mdogo unaoendelea.

"Tuko katika chumba chetu cha kulala ‘bedroom’ na nataka kuuliza watu wetu kulinda bedroom yetu dhidi ya watu wan je," Raila alisema.

Akizungumza baada ya kupiga kura katika shule ya msingi ya Old Kibra siku ya Alhamisi Raila alitoa wito kwa wananchi Kibra kudumisha amani.

"Tunataka watu wajiamuliye wenyewe…tunataka wafuasi wetu wote kuwa na amani hatutaki mtu yoyote kulalamika kwamba alitishiwa," alisema.

"Watu lazima waruhusiwe kutekeleza haki yao ya demokrasia. Natoa wito nyinyi wote mje mpige kura.."

Raila aliwaambia wenyeji hawakuwa wa piga kufanya. Alikuwa ameandamna na mkewe Ida na binti Rosemary Odinga.

Bernard Imran wa ODM anang’ang’ania kiti hicho kilichoachwa wazi kufuati kifo aliyekuwa mbunge marehemu Ken Okoth.

Jumla ya makarani 625 wanasimia uchaguzi huo.