Raila Odinga afanyiwa vipimo vya corona

Raila
Raila
Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga aliamua kufanyiwa vipimo kuhusiana na virusi hatari vya corona katika kituo cha utafiti cha KEMRI eneo la Mbagathi.

Baada ya kufanyiwa vipimo hivyo, Raila aliwataka wananchi kujitokeza na kufanyiwa vipimo kama njia ya kusaidia serikali kubaini idadi ya watu walioathirika nchini.

“A COVID-19 certificate is becoming an important document as we continue battling the pandemic,” alihimiza Raila.

Raila pia alizuru vituo mbalimbali vya kuwapima wakenya na kuwapongeza wahudumu wa afya kwa kuendelea kushughulikia maisha ya wakenya kuhusiana na virusi hivyo.