Raila Odinga alifanyiwa upasuaji kutokana na shida ya Neva- Familia yasema

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga alifanyiwa upasuaji wa kutokana na shida ya Neva ama Nerve Disorder katika milki za kiarabu  UEA.

Kulingana na taarifa iliyochapishwa kwa jarida la The Standart,Raila alifanyiwa upasuaji baada ya shida hiyo ya Neva kuleta tatizo katika mguu wake.

Mkewe kiongozi huyo Ida Odinga ambaye alifanya mahojiano na jarida hilo,alisema mumewe yupo vyema japo anahitaji muda wa kupata nafuu kikamilifu.

“He is in the United Arab Emirates-Dubai based International Hospital run by Germans. He has been successfully treated of a mild nerve disorder affecting one leg and not what has been alleged,”Ida.

Wakati uo huo alikashifu baadhi ya taarifa zilizokuwa zinaenezwa na wakenya kuhusiana na hali ya kiongozi huyo akiwataka wananchi kuepukana na taarifa kama hizo.

“Treat such rumours with utmost contempt and abhorrence. It’s not right to speculate on someone’s health,”

Familia ya kinara huyo pia imesema kwamba kinara huyo atakuwa anajea nchini chini ya wiki moja japo wakasisitiza ni sharti apate nafuu kwanza.