Raila Odinga amejificha Dubai si mgonjwa-Miguna Miguna Adai

Wakili Miguna Miguna amedai kuwa kinara wa chama cha ODM Raila Odinga si mgonjwa bali amejificha nchini Dubai. Kupitia kwenye mitandao ya kijamii ya twitter, Miguna alisema kuwa Raila ana hofu ya kuona ukweli kati yake na Uhuru Kenyatta.

Pia alisema kuwa Rila alifanya hivyo mwaka wa 2017 baada ya marudioa ya uchaguz mkuu wa rais alipoenda marekani kwa siku 10.

"Conman Raila Odinga is just hiding in Dubai and pretending to have lost his sight and gone blind but the truth is that he fears facing the reality that despot Uhuru Kenyatta has shafted him. He did the same and hid in New York in November 2017. ." Aliandika Miguna.

Usemi wake unajiri siku moja baada ya Junet mohamed na Hassan Joho kumtembelea Raila nchini Dubai.

Kinara wa ODM alisafiri kwenda Dubai kupokea matibabu ya upasuaji na kuendelea vyema baada ya upasuaji. Raila alikuwa na haya ya kusema;

"I'm feeling great. Strong and rejuvenated. I feel so good to be out of the hospital and to be getting this fresh air. I want to thank all my friends and supporters who have sent me messages of goodwill and prayers. This is why I have recovered so fast and it is wonderful." Alisema Raila kupitia kwa video.