Raila Odinga amtembelea gavana Laboso London

Kiongozi wa ODM  Raila Odinga  amemtemebelea  gavana wa  Bomet  Joyce Laboso  hospitali huko London Uingereza .Odinga aliandamana na balozi wa Kenya nchini Uingereza Manoah Esipisu .

 Wawili hao walimtakia Laboso  afueni ya haraka  wakati wa ziara hiyo .Haijafahamika Laboso anaugua nini lakini amechukua likizo ya matibabu kutoka shughuli zake kama gavana .

Kirui  amepepezea chini ripoti  kwamba gavana Laboso hajakuwa akitekeleza majukumu yake kwa ajili ya maradhi akisema kwamba amekuwa Nairobi akiendelea na kazi zake .

“ Amekuwa kazini wakati wote huo  na hayo  ndio tuayoweza kusema .. chochote zaidi ya hapo sasa ni mambo ya kibinafasi ambayo hatuzwezi kufichua’.