Raila Odinga azuru ngome ya William Samoei Ruto. Ni ziara ya kuzima TangaTanga?

hgu__1561897283_76439
hgu__1561897283_76439
Kiongozi wa upinzani chini Raila Amollo Odinga leo jumapili amezuru bonde la ufa. Raila alikuwa amealikwa kama mgeni mashuhuri katika hafla ya kusherehekea kustaafu kwa mwalimu Ruth Kiptoo iliyofanyika katika shule ya msingi ya Chebara. Ruth amehudumu katika Tume ya Kuajiri Walimu (TSC) kwa kipindi cha miaka 40.

Soma hapa:

Kiptoo ni mama mkwe wa mbunge wa Cherangany Joshua Kutuny.Wengine waliokuwa wamealikwa ni wakili na seneta wa Siaya James Orengo pamoja na mbunge wa Mbita Millie odhiambo.

Kutuny ni mojawapo ya wapinzani wa Ruto katika siasa za bonde la ufa. Ni wiki 2 tu zilipita ambapo Kutuny alisema kuwa ziara za Ruto za TangaTanga zinaonyesha dalili ya kumfanya aonekane kuwa atamrithi Uhuru Kenyatta japo akaonya kuwa juhudi zake hizo na kung'ang'ani nafasi hiyo ndiyo mapungufu yake kama kiongozi.

Uhuru na Raila sasa wameanzisha ziara ya pamoja nchini kuhubiri umoja na ushikamano huku wakipigia debe urafiki wao ambao ni maarufu kama "Handshake"

Soma hapa:

Ruto amekuwa akizunguka nchini na kuidhinisha miradi ya maendeleo. Ziara hizi zinaonekana kama juhudi za mchwa ili kukipata kiti cha urais mwaka wa 2022.

Msemaji wa ikulu Bi. Kanze Dena jumanne wiki hii alitangaza kuwa mpangilio wa ziara ya rais itakuwa inatangazwa kwa muda usio mrefu.