Raila Odinga kuwarai Maseneta kuunga mkono mfumo mpya wa ugavi wa fedha kwa kaunti

unnamed (38)
unnamed (38)
Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga sasa anapania kufanya kikao na Maseneta ili kuwarai kuunga mkono mfumo mpya wa uagvi wa pesa kwa kaunti 47 unaopendekezwa na hazina kuu ya taifa.

Odinga,Peter Kenneth na David Murathe wamefanya kikao cha faragha katika boma la katibu mkuu wa chama cha wafanyakazi nchini Francis Atwoli kama njia ya kutafuta suluhisho kwa mgawanyiko unaoshuhudiwa ndani ya seneti kwa sasa.

Mswada wa kujadili ugavi wa fedha katika bunge la seneti umeairishwa mara sita mfululuzo sasa baada ya maseneta kuupinga kwa kauli moja kuwa huenda baadhi ya majimbo nchini yakapoteza pesa nyingi ,hivyo kulemaza shughuli za maenfdelea.

Akizungumza na jarida la The Star,Kenneth amesema kuwa wamefanya kikao hicho ili kubaini namna ya kusitisha mgawanyiko unaoshuhudiwa kwa sasa ndani ya seneti.

Ameongezea kuwa Raila amehaidi kuwashinikiza maseneta kutoka mprengo wake ili kuuunga mkono mswada huo ,jambo ambalo amesema litafanikishwa kwa ushirikiano na kiongozi wa wachache James Orengo.

Ameongezea kuwa mazungumzo yao pia yameguzia maswala kuhusiana na handshake baina Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.

Kati maseneta 25 walioupinga mswada huo ,18 walikuwa wa mrengo wa Nasa unaongozwa na Raila Odinga wengine wakitokea katika chama cha Jubilee.

Wiki jana ,Kiongozi wa wengi Irungu Kang'ata alisema kuwa atahakikisha mswada huo unapasishwa wakati bunge hilo litakaporejelea vikao vyake Jumanne yaani hiyo Kesho.