Raila:Ripoti ya BBI inakaribia kutolewa,wanaoipinga ni wafisadi na lazima tuwashinde

Kiongozi wa ODM Raika Odinga amesema ripoti ya BBI Iko tayari kutolewa huku akilalamika kwamba kuna watu wanaopanga kuipinga ripoti  hiyo . Odinga amesema wanaoipinga ripoti hiyo ni  walionufaika na ufisadi na ukiukaji wa sheria .

Katika kinachoonekana kama kumlenga naibu wa rais  William Ruto ,Odinga amesema  wanaopinga ripoti hiyo wameanza kuwatia wakenya woga  na kuwahonga wakenya kutumia pesa  kando na kuchochea vita miongoni mwa wananchi .

Amesema wakenya wanafaa kuwakomesha watu hao dhidi ya kuzuia ustawi wa nchi .

Akionekana kuashirikia uwezekano wa kampeini kali kabla ya kura ya maoni kuhusu mapendekezo katika ripoti hiyo Odinga amesema miezi kadhaa ijayo  itakuwa makabiliano kati ya  walionufaika na ufisadi na wanaotaka kuleta mageuzi nchini kama vile kuleta nafasi za ajira  na kuboresha uchumi wa taifa .Amesema lazima  lazima wanaopigania maslahi ya Kenya wavishinde vita hivyo.