uhuruvisitsmoitomournjonathan

Rais Kenyatta amtembelea na kumfariji Rais Mstaafu Moi kufuatia kifo cha Jonathan Moi

Rais Uhuru Kenyatta leo alimtembelea Rais Mstaafu Daniel Arap Moi nyumbani kwake Kabarak, kaunti ya Nakuru, na kuwasilisha kibinafsi risala zake za rambirambi kufuatia kifo cha mwanawe Jonathan Toroitich Moi.

Alipowasili, Rais Kenyatta ambaye alilakiwa na Seneta wa Baringo Gideon Moi, alitia saini kitabu cha faraja kabla kufanya mkutano wa faragha na Rais Mstaafu Moi.

Rais alifariji familia ya Moi na akawahakikishia yuko pamoja nao na anawaunga mkono kikamilifu wakati huu wa kuomboleza.

Kiongozi wa Taifa alimsifu Marehemu Jonathan Moi, akisema alikuwa rafiki na ndugu yake.

Photo Credits: PSCU

Read More:

Comments

comments