Rais Kenyatta asema ripoti ya BBI iko tayari, ashauri Wakenya wafanye maamuzi ya busara

BBI
BBI

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kwamba ripoti ya Mpango wa Kuwaunganisha Wakenya BBI itakabidhiwa kwake siku ya Jumanne wiki Ijayo na kuwashuari Wakenya waisome kwa makini  kabla ya kuamua iwapo wataiunga mkono au kuipinga.

Rais alitoa wito kwa viongozi wa kisiasa kutahadhari wanapojadili ripoti hiyo akisema mpango huo haustahili kuwagawanya Wakenya.

Akizungumza alipoongoza sherehe ya nne ya kufuzu ya Chuo Kikuu cha Kibabii  katika Kaunti ya Bungoma, Kiongozi wa Taifa aliwahakikishia Wakenya kwamba atawashirikisha katika ripoti hiyo mara atakapoipokea.

Alielezea matumaini yake kwamba kupitia ripoti hiyo Wakenya watapata fursa ya kuboresha nchi kwa kuimarisha mfumo wa utawala.

Hayo yakijiri, machifu katika kaunti ya Taita Taveta wametakiwa kuanza kuwatambua watahiniwa wote waliofanya mtihani wa KCPE katika maeneo yao ili kufanikisha agizo la waziri wa elimu Prof. George Magoha la wanafunzi wote kujiunga na kidato cha kwanza.

Kamishna wa kaunti hiyo Rodah Onyancha kadhalika amewarai wazazi kushirikiana na machifu pamoja na wakuu wa shule katika zoezi hilo.
Ameonya wazazi dhidi ya kuwaoza mabinti zao mapema na kusisitiza kuwa kila mwanafunzi atapata nafasi ya kujiunga na shule ya upili mwaka ujao.

-PSCU na Solomon Muingi