Rais Kenyatta asimulia namna alivyomsomea mwanawe kwa kujaribu kuweka maisha ya nyanyake hatarini

uk
uk
Rais Uhuru Kenyatta akiwa kwa mahojiano na Nation amesimulia namna alivyomsomea mwanawe kijana ambaye aliamua kuhepa usiku kutoka kwa nyumba na kwenda kujivinjari wakiwa kaunti ya Mombasa pamoja na nyanyake Ngina Kenyatta wa Miaka 86.

Kiongozi wa taifa amesema baadhi ya familia yake walifungiwa katika kaunti ya Mombasa baada ya serikali kutangaza masharti mapya kwenye kaunti tano nchini ambazo zimeandikisha idadi kubwa ya maambukizi.

Kenyatta amesema baada ya kuarifia tukio hilo, alisomea mwanawe huyo japo hakutaja jina lake kwa kukosa kuwajibikia hali yake ya afya na ya wengine wakati huu ambapo virusi vya corona vimekithiri..

“I have a young man who was travelling to Mombasa with his mother when all of this [cessation of movement] happened, so they were caught out in Mombasa and because of these confinement rules we have put they can’t move back. Alielezea kiongozi wa taifa.

Uhuru anasema mwanawe huyu alikuwa na swala la kibinafsi ambalo alikuwa anataka kumfahamisha nyanyake Ngina Kenyatta japo akasema  hatua ya  kijana huyu kutoroka kwa nyumba usiku haingestahili kwani alikuwa anahatarisha maisha ya bibi huyo aliye na umri wa  miaka 86.

“He decided one day that he wants to go out and I asked him a personal question: ‘You have gone out, you have had your fun and enjoyed yourself, but now you have come back and you’re with your grandmother, who is 80 plus. If anything happens to your grandmother as a result of what you have done how will you live with yourself?” Alisimulia rais Kenyatta akiwa kwa mahojiano na Nation.

Uhuru akitumia mfano wa mwanawe amemtaka kila mkenya kuwajibika ipasavyo haswa wakati huu ambapo taifa linaendelea kusajili idadi kubwa ya maambukizi.

“It is that son of mine I was telling you… He has to ask himself: ‘Your grandmother’s life is in your hands… if something was to happen to her,  just because of one evening out to go see your girlfriend…” Aliongeza rais Kenyatta.

Akihutubia taifa mnamo Mei 24, rais Kenyatta alisema wakenya hawataendelea kuishi chini ya masharti makali japo akasisitiza umuhimu wa watu kuzingatia yale wanayoambiwa na wahudumu wa afya.

Katika mahojiano hayo vile vile, Uhuru alisema taifa linapokaribia kufungua uchumi wake wa kawaida kwa kuruhusu watu kurejelea shughuli zao za kawaida ni vyema kila mmoja awajibike ipasavyo.

“As we come closer to reopening our economy, there shall be a factor of personal responsibility because we have seen a second wave of this disease. Germany is a perfect example,” amesema Rais Kenyatta.

Aliongea haya rais Kenyatta.

“We will not continue with the lockdown and the curfew, I have told health officials and my ministers that they should start telling Kenyans that we cannot be under a curfew or lockdown forever… You have a responsibility to ensure you protect yourself, you should know that if you don’t obey the measures, you are not only endangering yourself, but those around you,”