"Rais Kenyatta haendi popote, yupoyupo, " asema David Murathe

murathe1
murathe1
David Murathe ameifungukia runinga ya Citizen kuwa kuna uwezekano mkubwa Rais Kenyatta akawa waziri mkuu mwenye mamlaka iwapo mapendekezo ya BBI yatapitishwa.

Tamko la kiongozi huyu linajiri baada ya Kenyatta kufanyia utani swala la kiti hiki cha waziri mkuu.

Katika kongamano la viongozi kutoka mlima Kenya, Uhuru alisema kuwa hawezi kubania nia ya kuwa waziri mkuu.

Chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga kinashinikiza kiti cha waziri mkuu kiwe na mamlaka zaidi.

“Rais Kenyatta  haruhusiwi tu kuwania urais tena lakini chini ya mfumo mpya unaotarajiwa kupitia kwa ripoti ya BBI, patakuwa na nafasi zaidi za uongozi," alisema Murathe.

"Hakuna chochote kitakachomzuia Rais ambaye ni kiongozi wa Jubilee kusimamia serikali kama Waziri Mkuu mwenye mamlaka, mradi tu chama hicho kiendelee kuwa kikubwa zaidi kwa idadi ya viongozi nchini Kenya,” alisema Murathe.