Rais Kenyatta na Mama wa Taifa waandalia watoto karamu ya sherehe za krismasi

Rais Uhuru Kenyatta na Mama wa Taifa Margaret Kenyatta leo waliandaa karamu ya sherehe za krismasi kwa ajili ya watoto wa wafanyakazi wa Ikulu na wa maafisa wa usalama wa vikosi vya ulinzi wa Rais.

Kutamatisha  karamu hiyo, Rais na Mama wa Taifa waliwaongoza watoto hao kukata keki, kuimba nyimbo za krismasi na pia kurusha fataki kuashiria msimu wa krismasi.