Rais Magufuli apendezwa na wimbo wa Sauti sol 'Extravaganza'

Wimbo wa sauti sol "extravaganza" umesifiwa na Rais wa Tanzania John Magufuli akisema kuwa wimbo huo kutoka kwa vijana hao, unampa msukumo.

Ni maneno ambayo aliyatamka kutoka kwa kinywa chake wakati alipokuwa akiwahutubia watanzania katika mkutano wa kuzindua mfumo mpya wa radar.

Watunzi wa wimbo huo "extravaganza" Sauti sol, wakizungumza na gazeti la The Star waliwashukuru sana bwana Magufuli kuwatambua vijana.

Bendi hiyo ikiongozwa na Bien alisema kuwa wana sababu ya kufurahi kwani ujumbe wa wimbo huo umeweza kufika kwa hadhira ya Tanzania. Aidha Bien aliongeza kuwa si jambo rahisi kutumia wimbo kueleza maadili.

Bien alisema kuwa iwapo wangekutana na Rais huyo wa Tanzania, wangemtia moyo kuendelea kufanya kazi nzuri katika nchi hiyo jirani, manake ni kwa faida ya raia wa nchi hiyo, kwani anatumia pesa ya walipaji kodi vizuri na haitaji msaada kutoka nchi zingine kinyume na nchi yetu.

Kwa sasa bendi hilo inashughulikia kanda ingine.