Rais mustaafu Mwai Kibaki alazwa tena

Rais mustaafu Mwai Kibaki amelazwa katika hospitali moja hapa jijini Nairobi chini ya wiki moja baada ya kuondoka hospitalini.

Rais huyo kwa zamani anasemekana kukimbizwa katika Nairobi Hospital siku ya Jumatatu jioni na kulazwa katika eneo la watu mashuhuri ambako anaendelea kupokea matibabu.

Hata ingawa hapakuwepo jamaa wa familia yake kueleza anachougua, rais huyo msataafu ambaye anakumbukwa sana kwa kukwamua uchumi wa taifa wakati wa uongozi wake, duru katika hospitali zasema kwamba Kibaki anatibiwa tatizo sawa na lile alilokuwa nalo mara ya mwisho alikuwa hospitalini.

Soma habari zaidi;

“Mzee yuko anashughulikiwa na madaktari. Amefanyiwa vipimo kadhaa kujaribu kubaini chanzo cha maumivu anayohisi,” duru zilisema.

Mwezi uliopita, rais huyo wa zamani alilazwa katika hospitali hiyo na kutibiwa kutokana na maumivu ya tumbo.

Kibaki mwenye umri wa miaka 89, alihudumu kama rais wa Kenya kati ya mwaka 2002-2013, akiwa rais wa tatu wa Kenya.

Amekuwa nje ya umma tangu alipostaafu baada ya hatamu mbili. Kibaki alipelekwa mjini London mwezi Septemba mwaka jana kwa matibabu kutokana na tatizo la goti.

Soma habari zaidi;

Hiyo ilikuwa ziara ya tatu ya matibabu kwa mzee Kibaki ambaye alisafirishwa mjini London mwaka 2002 baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani katika eneo la Machakos akiwa katika kampeni za uchaguzi mkuu.

Licha ya kwamba alikuwa amelazwa wandani wake wakiongozwa na kinara wa mpinzani Raila Odinga walimpigia dembe na akashinda uchaguzi wa mwaka huo na kuapishwa akiwa kwenye kiti cha magurudumu Disemba 30, 2002.

Soma habari zaidi;

DPP aagiza DCI na IPOA kuchunguza madai ya polisi kumdhulumu MCA Nairobi

Kibaki pia alipelekwa nchini Afrika kusini kwa matibabu mwaka 2016 alikotibiwa na kisha kurejea nchini.