Rais Uhuru akabidhiwa rasmi ripoti ya BBI, wananchi kupokea Jumatano

Uhuru Reading BBI
Uhuru Reading BBI

Rais Uhuru Kenyatta mnamo Jumanne amekabidhiwa ripoti rasmi ya BBI.

Hafla ya kuzindua ripoti hiyo imefanyika katika ikulu ya Nairobi.

Hata hivyo, uchambuzi wa ripoti hiyo utafanywa Jumatano utakapowekwa wazi kwa wananchi wote.

Miongoni mwa waliokuwemo katika halfa hiyo ni pamoja na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga, naibu wa rais William Ruto na maspika wa mabunge yote.

Jopo la maridhiano ya uwiano unaongozwa na Yusuf Haji lilisema kuwa ripoti hiyo ina maoni yote yaliotolewa na wananchi kote nchini.

Aidha Haji aliongeza kusema kuwa jopo hilo liliweza kupokea maoni kutoka zaidi ya viongozi 400 na wakenya kwenye kaunti zote.
Hata ingawa mapema ilisemekana kuwa huenda ripoti ingehairishwa kutokana na maafa ya zaidi ya watu 43 kaunti ya West Pokot.
Ripoti hiyo ya BBI ilikuwa imeratibiwa kukabidhwa rais saa saba mchana.
Na hata ilipofika saa tisa alasiri, haikuwa imefika ikuluni na kuzua wasiwasi  kutokana na subra kuhusu ripoti hiyo.
Rais amewaalika zaidi ya viongozi 100 kutoka kila kaunti kuhudhuri uzinduzi wa ripoti hiyo katika eneo la Bomas Jumatano.