Rais Uhuru atangaza!Kenya yaanza kuuza mafuta yake

tullow.1
tullow.1
Siku ya Alhamisi Kenya ilijiunga na Jumuiya ya Mataifa yanayouza mafuta ya petroli ulimwenguni.

Rais Uhuru Kenyatta alitangaza hatua hii muhimu katika historia ya taifa la Kenya alipoongoza mkutano wa baraza la mawaziri siku ya Alhamisi.

Habari zaidi:

“Kwa wakati huu sisi ni wauzaji wa mafuta ugaibuni. Mkataba wetu wa kwanza uliafikiwa leo mchana ukihusisha mapipa 200,000 ya thamani ya dola milioni 12 za Kimarekani,” Rais Kenyatta alisema.

Kenya imekuwa ikiendelea na shughuli za uchimbaji na kusafirisha mafuta kutika kaunti ya Turkana. Rais Mustaafu Mwai Kibaki alitangaza kupatikana kwa mafuta nchini Kenya mwaka 2012.

Changamoto hata hivyo zimekuwa kuyasafirisha mafuta hayo huku malori yakitumika kuyasafarisha kutokana na kutokuwepo kwa bomba la kuyasafirisha hadi bandari ya Mombasa ili yasafirishwe ughaibuni.

Habari zaidi:

“Nadhani tumeanza safari na ni juu yetu kuhakikisha rasilimali hizo zinatumika kwa njia bora kufanikisha taifa letu kimaendeleo na pia kuhakikisha tunamaliza umaskini,” kasema Rais Kenyatta siku ya Alhamisi.

Thamani ya mafuta ya Kenya inakadiriwa kuwa takriban shilingi trilioni 1,991.4.