Rais Uhuru Kenyatta aagiza wizara ya michezo kuanza matayarisho ya Olimpiki

Rais Uhuru Kenyatta aagiza wizara ya michezo kuanza matayarisho ya michezo ya Olimpiki ambayo ambayo imepangiwa kuanza mwaka ujao.

Huku akifungua uwanja wa Nyayo, rais alisifia kurudi kwa shughuli za michezo huku akisema ni ishara njema ya jinsi nchi hii inaweza kujikakamua na kujikaza katika nyakati zisizo za kawaida.

Rais pia aliahidi kuwa viwanja vingine nchini vitafanyiwa ukarabati pia ili magwiji weti wa kispoti wazidi kuonesha talanta zao kimataifa.

Rais pia aliagiza wizara ya michezo nchini kuhamasisha mafunzo dhidi ya utumizi wa dawa za kupasha misuli, upimwaji na pia kuripoti mara kwa mara baina ya wakimbiaji ili kuzuia utumizi wa bidhaa vilivyopigwa marufuku. Alisema ingawa visa vya matumizi ya madawa ni vichache, bado vinasumbua.