Rais Uhuru Kenyatta akutana na viongozi wa Magharibi kujadili maendeleo

Eb2pzWsWAAIOO9L-640x400
Eb2pzWsWAAIOO9L-640x400
Rais Uhuru Kenyatta alikutana na viongozi kutoka mkoa wa Magharibi katika jumba la Harambee ili kujadiliana kuhusu miradi ya maendeleo inayopaniwa kuanzishwa na serikali.

Kenyatta na viongozi hao walijadili kuhusiana na uwezo wa serikali wa kufufua kampuni ya kutengeneza sukari ya Mumias na Nzoia.

Kiongozi wa taifa aliwahakikisha viongozi hao kuwa serikali iko tayari kufufua kampuni hizo baada ya kamati ya watu 14 kuwasilisha ripoti yao.

Kama njia ya kufufua sekta ya uchumi kwa wakaazi wa Magharibi, serikali imechapisha mswada wa kuratibu uuzaji wa sukari nchini kama njia ya kuzuia sukari ya magendo kuuzwa maeneo tofauti nchini.

Baada ya mkutano huo, kiongozi wa taifa aliwakabidhi viongozi hao basi la kubeba watu 52 na ambalo litatumika kuwabeba wachezaji wa timu ya Nzoia.

Mkutano huo ulihudhuriwa na magavana  Wycliffe Oparanya (Kakamega), Sospeter Ojaamong (Busia), Wycliffe Wangamati (Bungoma), Wilbur Ottichilo (Vihiga) na Patrick Khaemba (Trans-Nzoia).

Viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni waziri wa Ugatuzi Eugene Wamalwa na katibu wa COTU Francis Atwoli.