Rais alikuwa amengojewa na mawaziri kadhaa ili kutoa taarifa kuhusu virusi vya Corona ambapo alithibitishwa kugunduliwa kwa visa viwili zaidi vya ugonjwa huo baada ya kisa cha kwanza kuripotiwa tarehe 13 machi . Gari hilo lililombeba rais halikuwa bdenera maalum ya rais au bendera ya taifa na pia Uhuru hakuwa na msaidizi ambaye huwa nyuma yake . Wakati wa hafla hiyo rais alitangaza mikakati kadhaa iliyochukuliwa na serikali kuzuia maambukizi zaidi ya virusi hivyo ikiwemo kufungwa kwa shule zote .
Serikali pia imepiga marufuku kuingia nchini kwa raia wa kigeni kutoka nchi zilizoripoti visa vya Corona .Wakenya na raia wa kigeni wanaotaka kuja nchini watahitajika kujitenga kwanza kwa siku nne au katika vituo vya afya vya umma .Serikali pia imewaagiza wakenya kupeuka Mikutano ya hadhara ,hafla za makanisa na maeneo yenye watu wengi kwa siku 30 zijazo . Biashara ,kampuni za kibinafsi na mashirika ya umma pia zimeagizwa kuwaruhusu wafanyikazi wao kufanyia kazi nyumbani isipokuwa wale wanaofanya kazi zinazowahitaji kwenda afisini .
Rais Uhuru Kenyatta pia amewarai wakenya kutotumiapesa taslimu kufanya ununuzi bali kuzingatia kutumia mifumo ya malipo ya kutumia simu au kadi . Hospitali na duka za jumla zimetakiwa kutoa maji na sabuni kwa wateja ili waweze kuosha mikono yao.