Rais wa Botswana na mawaziri wake wawekwa chini ya Karantini

Masisi
Masisi

NA NICKSON TOSI

Rais wa Botswana Mokgweetsi Masisi, mawaziri wake na wabunge wamewekwa chini ya karantini baada ya mhudumu wa afya aliyewafanyia vipimo vya kutathmini iwapo wana virusi vya Corona, kupatikana na virusi hivyo.

Mbunge mmoja wa Botswana amesema kuwa wabunge wote wameamrishwa kujitenga kwa siku 14 baada ya kuhudumiwa na mhudumu huyo wa afya  Jumatano na ambaye alipatikana na virusi hivyo.

Bunge la taifa hilo lilijawa na wasiwasi Alhamisi baada ya taarifa hizo kujiri, Shirika la AFP limeripoti.

Kufikia sasa taifa hilo limedhibitisha visa 13 vya maambukizi.

 MHARIRI: DAVIS OJIAMBO