Rais wa zamani wa Jamhuri ya Congo Jacques Joaquim Yhombi-Opango, amefariki jijini Paris baada ya kupatikana na virusi vya Corona .
Alikuwa na umri wa miaka 81. Familia yake imesema alikuwa akiugua hata kabla ya kupatikana na virusi vya corona .
Yhombi-Opango aliongoza Congo-Brazzaville kutoka mwaka wa 1977 hadi mwaka wa 1979 alipoondolewa madarakani na rais wa sasa wa taifa hilo Denis Sassou Nguesso. Aliwekwa jela kwa miaka kadhaa kabla ya kuanzishwa kwa siasa za vyama vingi mwaka wa 1991 alipohudumu kama waziri mkuu kisha baadaye vita vya wenyewe kwa wenyewe vikazuka mwaka wa 1997. Alikimbilia mafichoni nchini Ufaransa kabla ya kuruhusiwa kurejea nyumbani miaka 10 baadaye .