Rasmi sasa! Wakaazi wa Murang'a kuanza kuhudumiwa baada ya chumba cha kuangazia Corona kufunguliwa

EXUcrYwXQAI4Lus
EXUcrYwXQAI4Lus
NA NICKSON TOSI

Ni afueni kwa wakaazi wa kaunti ya Murang'a baada ya uongozi wa jimbo hilo kufungua kituo kilichojengwa kwa siku 21 kuanza kutoa matibabu na hata kuwapima wakaazi wa eneo hilo kuhusiana na virusi hatari vya Corona.

Kituo hicho maalum na ambacho kimewekwa mashine maalum kama vile ICU sasa kitakuwa na wajibu wa kuwapokea wagonjwa kutokwa kaunti jirani za Mkoa wa Kati.

Kituo hicho kilifunguliwa baada ya viongozi wa kidini kuombea wote watakaokuwa wanahudumu hapo.

Sekta ya afya imekuwa na changamoto kuu kwa serikali za kaunti ambapo baadhi ya wananchi wamekuwa wakilazimika kusafiri hadi jiji kuu la Nairobi kupata tiba.

Kituo hicho sasa kina uwezo wa kuwalaza wagonjwa kutoka kaunti zingine eneo hilo.