Ratiba ya miji atakayozuru sonko wa masonko wiki hii. Mji wako ni upi?

Ratiba kamili ya miji atakayotembelea sonko wa masonko wa Redio Jambo imewekwa wazi kama mlango wa kanisa ili mashabiki wajue kwa kiuhalisia wanapaswa wamsubiri maeneo gani na wakati upi katika wiki hii.

Leo jumatatu sonko ashamwaga hela lukuki tayari katika kaunti ya Kiambu na kuzamia kaunti ya Nyeri. Kupitia swali mboga sana la kuitambua “The Phrase That Pays”, msikilizaji anatuzwa shilingi elfu moja.

Kwa kutengeneza bango na kuandika Redio Jambo Ongea Usikike, mshindi anatuzwa elfu 5 pesa taslimu.

Soma hapa pia:

Kesho sonko huyu ataanza ziara yake mji wa Nyeri na baadaye alasiri kukita kambi maeneo ya Mwea. Msururu huu wa kutembelea miji mbalimbali utafikia maeneo ya Kirinyaga , Embu ,Meru na hatimaye Murang'a ijumaa.

Pata uhondo:

Sio mara ya kwanza kituo hiki kufika vijijini na mjini wanakosikiliza mashabiki wao. Nia na azma kuu ni kuwatuza mashabiki wake kwa kuwa balozi wazuri kokote nchini.