Rayvanny afunguka A-Z kisa cha kutemwa na mkewe, asema sio kiki

jay2_1024x996__1574849292_80518
jay2_1024x996__1574849292_80518
Staa wa mkwaju wa Tetema, Rayvanny amefunguka A-Z kuhusu kutemana na mkewe Fahy Vanny.

Haya yanajiri baada ya mkewe kumuandikia ujumbe huu ,

“Hesabu mimi na Jay amefariki kwenye maisha yako. Nitapigana na nitashinda. Sitakosa pesa ya kula. Ila mimi na Jay hesabu kuwa tumekufa kwenye maisha yako,” aliandika Fahy katika mtandao wa Insta.

Aidha, Rayvanyy amesema kuwa kuachana na mkewe sio kiki kwani bado anafanya vizuri katika soko la sanaa Afrika mashariki.

https://www.instagram.com/p/B5TPAeKABeh/

Staa huyu anahusishwa na skendo ya kuchepuka na mrembo Nana aliyeonekana kwenye kichupa cha video ya I Love You.

"Sina ufahamu wa kiki. Naishi maisha yangu. Nikidondosha ngoma mashabiki zangu huipokea freshi. Ulichokiona ndicho..." Alisema Rayvanny.

Msanii alikana kutoka kimapenzi na Nana.

"Sipo kwenye mahusiano na Nana, tena ana mahusiano yake ambayo nayaheshimu sana sana.Kichupa ni kizuri kwani kinaonyesha ukweli na mapenzi yapo. Nilitaka video hiyo iwe jinsi ilivyo.." Rayvanny aliongeza.