rayvanny

Rayvanny akanusha madai ya kutaka kujiuzulu katika label ya wasafi

Rayvanny amekanusha madai yanayo muhusisha na kutaka kuigura label ya wasafic classic baada ya Harmonize kujiondoa. Hivi majuzi, Mkali wa konde boy, Harmonize alijiuzulu kutoka label hio na kuanzisha label yake ya ‘Konde Gang’.

rayvanny-

Rayvanny ambaye amekuwa akiutetemesha ulimwengu na kibao chake, Tetema alisajiliwa na label ya wasafi clasics mwaka wa 2016 mwaka mmoja baada ya Harmonize. Rayvanny amesema kuwa wakati wa kujiuzulu kutoka kwa label hio haujafika  na bado yeye anawahitaji.

Harmonize aiandikia barua Wasafi akitaka kujiuzulu kirasmi

“Mimi nina meneja wangu,mlinzi wangu pamoja na produza ambao mimi hufanya kazi nao kila siku. Hata hivyo mimi bado naamini kuwa nahitaji label hio yao kwani wameniinua kwa miaka mitatu sasa.”

Tangu ajiunge na label hio, Rayvanny ameachilia vibao sita vilivyo utetemesha ulimwengu.

“Kwa sasa mimi siwezi sema kuwa nahitaji kuanza kufanya mambo yangu kivyangu na kwa sababu sijiwezi kwa sasa hivi. Nahitaji wakati wangu wa kujiuzulu hapo ukifika kila mtuu atakua anajua sasa nina uwezo wa kujisimamia kivyangu.”

Kulingana naye Rayvanny, Wasaniii wote wa wasafi wanahitajiana na hivyo haoni haja ya kujiuzulu.

Soma Mengi hapa

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments