Rayvanny_and_girlfriend__1569576864_85873

Rayvanny aweka wazi taarifa za kusaliti Mkewe Fayma kwa Elizabeth Lulu

Staa kutoka usafini WCB Rayvanny amefunguka mwanzo mwisho kuhusu tuhuma za kuchepuka.

Ubuyu kutoka Bongo ulihoji kuwa kuna dalili za mkali huyu kuwa anatoka kimapenzi na muigizaji Lulu.

Elizabeth Lulu ni mwanamitindo nchi jirani ya Tanzania aliyewahi kufungwa jela kwa kosa la kushiriki katika mauaji.

Soma hadithi nyingine:

Swaleh Mdoe atokwa na povu, siasa za uanahabari zimemchosha

Katika mahojiano Rayvanny alikana taarifa hizo,

“Unapomsema Lulu na unapomsema Rayvanny unaongelea familia…”

“Lulu yuko na familia yake, mimi niko na familia yangu…”

“Kwa hiyo unaposema kitu chochote kuhusiana labda mimi na Lulu kaa ukijua kwamba kuna sumu ambayo unaitengeneza ambayo ni kubwa sana.”

Taarifa za Rayvanny kuchepuka na Lulu ziliteka anga baada ya staa huyu kualikwa katika sherehe ya kuzaliwa kwake Lulu.

Kipande cha video kilichosambaa cha Rayvanny na Lulu kiliwafanya mashabiki kushuku uwepo wa mahusiano.

Soma hadithi nyingine:

Robert Mugabe azikwe Heroes Acre au Zvimba, suluhu ya mzozo yatolewa

Rayvanny amesema kuwa anaheshimu sana familia ya Lulu huku akisema kuwa taarifa hizi zilimuweka katika matatizo na mke wake Fayma.

“Mimi nina familia yangu ambayo naiheshimu sana Lulu mahusiano yake na familia yake ambao yeye anaiheshimu…”

“Mimi naheshimu sana. mimi nilienda kwenye party yake as a guest kama ninavyoalikwa sehemu zingine na kwa sababu tu ni Lulu na mimi watu wakaanza kutengeneza story. ”

“Ni vitu vya mitandao. Ni vitu ambavyo viliniletea mimi matatizo kwa mwanamke wangu.’

Soma hadithi za Abraham Kivuva

Photo Credits: courtesy

Read More:

Comments

comments