Rayvanny na Mbosso wampa shavu kavu Harmonize. Ushikaji haupo tena

3aR21lQKmZHarmonize2__1567068795_46720
3aR21lQKmZHarmonize2__1567068795_46720
Stima za ushikaji zinaonekana kuzima ghafla kati ya Harmonize na dogo zake waliokuwa katika lebo moja. Hii ilidhihirika jana baada ya Harmonize ambaye aliwasilisha barua ya kutoka usafini na kuonekana na mikakati ya kuanzisha lebo yake ya Konde Gang.

Soma hapa:

Harmonize aliposti ngoma za Rayvanny na Mbosso, Remix ya Tetema na Shilingi. Kama ilivyo desturi, wawili hawa wangeposti ngoma yake mpya na Eddy Kenzo Inabana kama kuonyesha kuipa nguvu sanaa yake ila wakakosa.

Soma mengine hapa:

Harmonize ameanzisha lebo yake Konde Gang ambayo anapania kuwasaini mastaa wengine wa muziki. Aidha, katika mahojiano Meneja wa WCB Babu Tale alisisitiza kuwa chochote Harmonize atakwenda kuanzisha kinachohusiana na burudani, kutakuwepo na pato itakayokuwa inaingia Wasafi.

Soma mengine hapa:

Lebo ya WCB imedondosha ngoma Shilingi ya Mbosso akimshirikisha Reekado masaa 5 baada ya Harmonize kutoa. Hii inaweza kutafsiriwa kama njia moja ya kufunika ngoma ya Harmonize. Mondi pia anatarajiwa kudondosha ngoma yake muda usio mrefu ili kuonyesha ubabe katika tasnia ya muziki wao.