eden hazard

Real Madrid imekubali kumnunua Eden Hazard kwa pauni milioni 88

Real Madrid imekubali kumnunua kiungo wa Chelsea Eden Hazard kwa pauni milioni 88 na marupurupu mengine.

The blues walikua wanaitisha takriban pauni milioni 130, kwa raia huyo wa Ubelgiji ambaye amesalia na mwaka mmoja kwenye mkataba wake.

Hazard, alitaka kuondoka Stamford Bridge baada ya kufunga mabao mawili na kuwanyuka Arsenal 4-1 katika fainali ya ligi ya Uropa wiki iliyopita.

Atakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Los Blancos wanapotafuta kujijenga kabla ya msimu mbaya.

Kwingineko, FIFA imethibitisha kua rais wa shikisho la soka barani Afrika Ahmad Ahmad anahojiwa na mamlaka nchini Ufaransa. Taarifa kutoka FIFA zinasema kua anahojiwa kuhusiana na madai dhidi ya uongozi wake wa CAF.

Taarifa hio pia inasema FIFA haiwezi kusema mengi zaidi kuhusiana na suala hilo.

Photo Credits: Daily Express

Read More:

Comments

comments