Real Madrid yatajwa kuwa klabu ya soka yenye dhamana ya juu

Miamba wa soka nchini Uingereza Manchester United imeshuka kwenye orodha ya klabu zenye dhamana ya juu zaidi ulimwenguni kutoka nafasi ya pili hadi nafasi ya sita.

Kufuatia Msururu wa matokeo duni msimu uliopita,United imejipata katika hali ya sitofahamu kwenye soko ya hisa ulimwenguni.

Kwa sasa Klabu ya Real Madrid inaongoza orodha ya vilabu vya soka Ulimwenguni huku Barcelona ikifuatia katika nafasi ya pili. Klabu ya ligi kuu ya Marekani, (NFL) inaongoza kwenye nafasi ya kwanza kwa dhamana ya billioni tano huku New York Yankees ikifuata.

Real Madrid yatajwa kuwa klabu ya soka yenye dhamana kuu zaidi ya kitita cha billioni nne nukta sita.

New York Knicks inafuata Barcelona katika nafasi ya tano kwa dhamana ya billioni nne huku Manchester United ikija katika nafasi ya tatu kwa dhamana ya billioni tatu nukta.