RED CARD:Pigo kwa watoto wanaozaliwa na mjane baada ya mume kufariki

   Watoto wanaozaliwa na wajane  miezi tisa baada ya waume zao kuaga dunia  hafawai kurithi mali  ya  marehemu .Mahakama imesema  watoto hao hawafai  kuchukuliwa kama wa   marehemu kwani hakuwa akiwatunza kama watoto wake kabla ya kifo chake .

 Mkusanyiko wa Habari na Matukio Muhimu 

 Mahakama  siku ya  jumatatu itasikiza kesi inayopinga   zezi la kumwajiri afisa mkuu mpya wa tume ya IEBC . Pande husika katika kesi hiyo zimetakiwa kuwasilisha maombi  huku korti ikishikilia kwamba  agizo la kuzuia kuajiriwa kwa afisa mkuu mtendaji bado lipo . kesi hiyo iliwasilishwa mwezi uliopita na  chama cha mawakili .

 Dennis Itumbi  ameachiliwa  kwa dhamana ya shilingi laki moja  pesa taslimu .hata hivyo ameagizwa kuripoti  katika kituo cha polisi cha muthaiga  mara mbili kwa wiki  kabla ya kesi hiyo kutajwa tarehe 22. Alikamatwa kuhusiana na  barua iliyodai kuwepo njama ya kumwua nairobu wa rais William Ruto.

Wakati huo huo baadhi ya wabunge wamesifu uamuzi wa mahakama kumwachilia Itumbi kwa dhamana  wakisema vitisho vinatumiwa ili kuwazuia wafanyikazi wa serikali kutekeleza majukumu yao .wanaitaka mahakama kumruhusu Itumbi kucheza ushahidi wa video  na sauti ili kuthibitisha kwamba kuna njama ya kumwangamiza Ruto.

Wakenya zaidi wanatazama runinga  na idadi ya vituo vya televisheni imeongezeka  tangu uhamisho wa  mtangazo hadi  mfumo wa kidijitali .Ripoti mpya  imesema hilo limetokana na kuwepo vya  ving’amuzi vingo vya bei rahisi .

Watu wanaomiliki bunduki kinyume cha sheria hasa katika sehemu zinazokumbwa na visa vya wizi wa mifugo huko rift valley  wameatakiwa kutumia msamaha uliotolewa na serikali kuzisalimisha . Mratibu  wa eneo la rift valley Edward Mwamburi   amesema huduma ya polisi imepigwa jeki na kuwasili kwa maafisa elfu 23 wa AP ili kufanikisha msako dhidi ya silaha haramu .

Fedha zaidi zinahitajika katika kaunti ili kutoa uhamasisho  wa kuzuia utumizi wa dawa za kulevya .mwakilishi wa akina mama wa kiambu  Gathoni Wamuchomba  amesema  kampeini za uhamisho zinafaa kufanywa  katika shule za msingi kwa wanafunzi wa gredi ya pili .

Waziri wa elimu   George Magoha  ameagiza uchunguzi kufanywa dhidi ya madai ya matesio dhidi ya wanafunzi katika shule ya Nairobi  . magoha amesema anataka kufahamu  wanaotekeleza ,atesi hayo na hatua kuchukuliwa .Anataka ripoti ya uchunguzi huo kufikia wiki ijayo.

  Madaktari huko Mandera  wamefutilia mbali mgomo wao  na kumaliza siku sita za mahangaiko  ya wakaazi ambao wametatizika kupata huduma za matibabu .katibu wa tawi la muungano wao Ibrahim Maalim amesema wameafikia mkataba mpya na serikali ya kaunti hiyo.

  Jopo la majaji watatu limeteuliwa na jaji mkuu David maraga  kusikiza kesi iliyowasilishwa kupinga hatua ya wabunge kutaka kulipwa marupurupu ya nyumba ya shilingi elfu 250 kila mwezi .majaji  Pauline Nyamweya, Weldon Korir na  John Mativo  ndio watakaosikiza kesi  hiyo iliyowasilishwa na tume ya mishahara .

Aliyekuwa  mwakilishi wa wadi ya  Isukha central  Richard Muchesia amejiua baada ya kumwua mkewe kwa kumpiga risasi katika eneo la Oangata rongai kaunti ya kajiado .Polisi wanasema wamesema wameanzisha uchunguzi kuhusu  tukio hilo

Serikali imejitolea  kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari  kupitia  hatua yake ya kuendelea kuunga mkono  tafiti za wanaotumia vyombo vya habari . waziri wa ICT Joe Mucheru  amesema wizara hiyo italipa pesa inazodaiwa  na kuwekeza katika teknolojia ya kisasa ili kuhakikisha kwamba huduma za vyombo vya habari zinamfikia kila mtu .

  Mwenyekiti wa Maendeleo ya wanaume Nderitu Njoka  amependekeza kwamba  cheti cha ndoa kitolewe kwa wanandoa baada ya  kuishi pamoja kwa mwaka mmoja  ,kwa ajili ya ongezeko la la visa vya mauaji ya wanandoa . pia amewashauri wanaopendana kutafuta ushauri kwa wataalam ili kusuluhisha matatizo yao  badala ya  kutumia ghasia .

   WANAUME   ambao hudhulumiwa na wake zao  hawafai kuona haya kujitokeza hadharani na kuwaripoti  . mwenyekiti wa maendeleo ya wanaume nderitu Njoka  amesema  sheria haifai kuwapendelea wanawake wanaowadhulumu waume zao kwani wanaume pia ni waathiriwa wa dhulma za kinyumbani .

Wasimamizi wa shule wanafaa kuzisikiliza lalama za wanafunzi ili kuepuka visa vya rabsha shuleni .mtalaam wa masuala ya elimu Eugen Ojiambo  amesema wakati mwingi wasimamizi wa shule huwa hawawahusishi wadau wote kushughulikia  masuala yalioibuliwa na wanafunzi .

 Idadi ya magezeti ya kila siku yanayouzwa nchini imekua ikupungua  .Ripoti kuhusu vyombo vya habari imeonyesha kwamba kumekuwa na upungufu wa asilimia 33 wa kiasi cha magazeti yanayouzwa nchini tangu mwaka wa 2013 . ingawaje redio husikizw ana watu wengi ,watu hungoja kusoma magazeti ili kuthibitisha  waliosikiza au kutazama katika runinga .